Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti wa ukatili wa kijinsia, ndugu wanyooshewa kidole

44079 Pic+ukatili Utafiti wa ukatili wa kijinsia, ndugu wanyooshewa kidole

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Dawati la Jinsia la Polisi Tanzania, Mary Nzuki amesema tafiti zao zinaonyesha waliofanya vitendo vya ukatili kwa watoto ni ndugu na watu wa karibu wanaoshinda nao kila siku.

Amesema nyumbani panapoonekana ndio salama kwa watoto sio salama tena.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya ulinzi wa  mtoto dhidi ya ukatili wa kingono zinazo endeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo Februari 27,2018 Nzuki amesema hali sio shwari kwa watoto.

"Taarifa zetu zinaonyesha wanaofanya haya matukio ni wajomba, kaka, baba mzazi, jirani na wapoatu wa karibu kabisa na watoto, nyumbani tulikodhani salama sio salama tena lazima kuchukua hatua," amesema.

Amesema wazazi na walezi ndio wanapaswa kuwa watu wa kwanza kabisa kuhakikisha mtoto analindwa.

"Wazazi mmekua bize sana, mkirudi nyumbani  mmechoka hata nafasi ya kuzungumza na mtoto hakuna, fuatilieni nyendo za watoto muwajue rafiki zao," amesema.

Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi amesema ili kuvunja ukimya mzito kwenye jamii kutokana na kasi ya matukio dhidi yao mengi yakiwa ya ngono.

Amesema kampeni hiyo ya muda mrefu itasaidia kuiamsha jamii kuhusu suala la ulinzi wa mtoto.

 

"Watoto wanandoto nyingi zitafikiwaje kama wanabakwa na kulawitiwa, hali sio mbaya kwa wa kike tu hata wakiume hali sio nzuri," amesema Liundi.

 

Mwisho.



Chanzo: mwananchi.co.tz