Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usafiri wakwamisha abiria Manyara

33087 Manayara+pic Tanzania Web Photo

Sun, 23 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Adha ya usafiri imewakumba abiria wanaokusudia kusafiri leo Jumapili Desemba 23, 2018 kutoka mjini Babati mkoani Manyara kwenda maeneo mbalimbali kwa ajili ya mapumziko ya siku kuu za mwisho wa mwaka. 

Abiria wengi hupenda kutumia mabasi yanayoanzia safari zake mjini Moshi na Arusha kwenda mikoa ya Kati na Kanda ya Ziwa ambayo yanafika Babati yakiwa yamejaa.

Wakala wa mabasi aliyejitambulisha kwa jina la Godfrey Maasay amesema yapo mabasi machache yanayoanzia safari zake Babati.

"Kipindi hiki tumeshuhudia pande zote zikikabiliwa na changamoto ya usafiri, wakati wa nyuma tulizoea abiria wanaokwenda Kilimanjaro lakini sasa hivi tunaona idadi ya abiria wanaolekea Dodoma, Mwanza na Iringa," amesema Maasay.

Jeni Mushi abiria anayekwenda mjini Moshi amesema amekuwepo kituoni hapo tangu saa 12:30 asubuhi na matumaini ya kupata usafiri yanapotea.

Baadhi ya wapiga debe walionekana wakitafuta abiria kwa ajili ya magari binafsi yanayokwenda Dodoma na Singida.



Chanzo: mwananchi.co.tz