Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usafi wa mazingira Sengerema sasa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi

FDGFFXF Usafi wa mazingira Sengerema sasa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi

Sat, 9 Dec 2023 Chanzo: Mwananchi

Wakazi wa Wilaya ya Sengerema wameagizwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yanayowazunguka kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema, Cuthbert Midala leo Desemba 9, 2023 wakati wa usafi wa mazingira katika eneo la Hospitari ya Wilaya ya Sengerema ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika uliopatikana Desemba 9, 1961.

Jamhuri ya Tanganyika iliyopata Uhuru Desemba 9, 1961 iliungana na Zanzibar kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 26, 1964, miezi michache baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Katika utekelezaji wa lengo la usafi wa mazingira, Midala amesema uongozi wa Serikali Wilaya ya Sengerema umewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya vijiji/mitaa, kata hadi wilaya kuwaongoza wananchi kufanya usafi katika maeneo yote ya huduma za umma ikiwemo zahanati, vituo vya afya, hospitali, shule na maofisi kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru.

"Wilaya ya Sengerema, tumeadhimisha miaka 62 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira maeneo ya huduma za afya katika halmashauri zote za Sengerema na Buchosa; shughuli hiyo imeshirikisha viongozi pamoja na wananchi nah ii itakuwa endelevu kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi,’’ amesema Midala

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Binuru Shekidele amesema kupitia maadhisho hayo, uongozi wa halmashauri umeuhamasisha umma kushiriki shughuli ya usafi kila mtu katika mazingira yake.

Catherine John, mkazi wa mjini Sengerema ameshauri usafi wa mazingira katika maeneo na ofisi za umma kuwa jambo endelevu badala ya kufanyika nyakati za maadhimisho ya kitaifa.

Chanzo: Mwananchi