Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upepo waua mmoja, nyumba 100 zaezuliwa

Kimbunga Upepooo Upepo waua mmoja, nyumba 100 zaezuliwa

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upepo mkali ulioambatana na mvua umeezua nyumba zaidi ya 100 na kusababisha kifo cha mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la Matias Nkomela mwenye umri wa miaka 73 katika kata ya shabaka wilaya ya Nyangh’wale mkoani Geita.

Wakizungumza nasi, wahanga wa tukio hilo wamesema usiku wa kuamkia Jumatatu baadhi yao walilazimika kulala nje kutokana na nyumba zao kuharibiwa na upepo.

“Jana jioni lilijitokeza wingu baada ya muda mfupi ukaanza kuvuma upepo tukawa tumekimbilia ndani mi na kijana wangu mdogo mara ghafla tukasikia kitu kinaanguka.

“Nikasema nyumba inaanguka mwanangu mwanangu akaniambia tukimbilie wapi nikamwambia tutoke ndani twende nje kuja kuangalia tukaona nyumba nzima imejaa vumbi,” amesema Ester Lukebela mkazi wa kata ya Shabaka.

Diwani wa kata hiyo Kalimu Hamis Chasama akithibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema upepo huo pia umesababisha maafa kwenye taasisi za serikali.

“Kwenye kata yangu ni nyumba nyingi ambazo zimeezuliwa na upepo kama mia moja na kitu kwa taarifa nilizopata mpaka sasa lakini pia kuna kwenye taasisi za serikali kama choo cha shule ya msingi Lubado kimeezuliwa.

“Darasa moja shule ya msingi muhama limeezuliwa lakini pia jengo moja la kununulia pamba katika kijiji cha muhama nalo limeezuliwa,” amesema Kalim Hamis Chasama Diwani wa Kata ya Shabaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live