Butiama. Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara nchini Tanzania wameiomba Serikali kutoa elimu ya upandaji miti ili kusaidia madhara yanayotokana na upepo mkali kupungua.
Wakizungumza na Mwananchi leo Jumanne Oktoba 15, 2019 wananchi hao wamesema sehemu kubwa ya nyumba zilizoathirika na upepo mkali uliotokea usiku wa kuamkia jana Jumatatu Oktoba 14, 2019 unatokana na kutokuwapo kwa mti ya kutosha.
Yasinya Warioba mkazi wa Butiama ambaye nyumba yake imeezuliwa amesema mpaka sasa amejihifadhi kwa ndugu yake baada ya nyumba yake kuezuliwa na upepo.
Mkuu wa wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi amesema mpaka sasa kuna majeruhi wawili wote ni watoto wa mwaka mmoja na wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara.
Amesema nyumba zaidi ya 49 na makanisa mawili yakiezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyotokea Oktoba 13, 2019.
Nyamubi amesema tukio limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 14, 2019 ambapo mpaka sasa hakuna taarifa ya kifo tofauti na majeruhi hao wawili.
Pia Soma
- Rais Zuma kukata rufaa dhidi ya kesi yake ya ufisadi
- Profesa Ndalichato atoa maagizo kwa katibu mkuu wizara ya elimu
- Tasupa watoa masharti ununuzi wa alizeti Tanzania
Mkuu huyo wa wilaya amesema kwa wote waliopata changamoto katika mvua hiyo tayari jitihada mbalimbali zimeshafanywa na kila kitu kimeenda sawa.