Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upepo waezua nyumba 13 Masasi

Upepo Pic Data Upepo waezua nyumba 13 Masasi

Tue, 25 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Upepo mkali ulioambatana na mvua umeezua nyumba 13 katika mtaa wa Nyasa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumanne Januari 25, 2022 Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa huo, Edward Hokororo amesema kuwa upepo huo ulianza usiku wa kuamka leo na kusababisha baadhi ya wakazi wa eneo hilo kushindwa kulala.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Ibrahim Chiputura amesema kuwa wanafanya tathmini kujua madhara yaliyotokana na upepo huo.

“Hatuwezi kuyasema kuwa ni kiasi gani kwa sasa lakini tunafanya upembuzi ili kujua kiasi cha athari na nini kimeathirika zaidi ya nyumba kutoka mapaa na zingine kuangukiwa na miti ndio tutatoa taarifa baada ya tathmini” amesema Chiputura

Meneja wa Hali ya Hewa Kanda ya Kusini, Daudi Almas amesema kuwa uwepo wa upepo huo umesababishwa na kitoto cha kimbunga kilichokuwa kinavuma kutoka nchini Madagascar kuelekea Msumbiji.

“Kimbunga kidogo yaani unaweza kukiita kimbunga mtoto kilipewa jina la Ana kilitokea Madagascar akasogea kwetu kidogo lakini jana ndio upepo ulikuwa mkali sana kilimita 50 kwa saa,

“Mamlaka ya hali ya hewa huwa tunatoa taarifa mapema wananchi wanapaswa kuwa makini na kufuatilia utabiri wa hali ya hewa” amesema Almas

Chanzo: www.mwananchi.co.tz