Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upatikanaji huduma maji Ludewa wafikia asilimia

Kero Majipic Upatikanaji huduma maji Ludewa wafikia asilimia

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali wilayani Ludewa mkoani Njombe inatekeleza miradi saba ya maji ambayo inatarajiwa kuongeza huduma ya upatikanaji wa maji safi kutoka asimia 74.3 hadi asilimia 79.7 eneo la vijijini na kufikia asilimia 100 kwa wakazi wa Mji wa Ludewa.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji na kusisitiza kuwa ni azma ya Rais Samia Suluhu Hassan juu ya kumtua mama ndoo kichwani.

Amesema Rais Samia anataka kila mwananchi apate maji safi na salama na kusisitiza umuhimu wa uelimishwaji wa jamii juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji sambamba na utunzaji miundombinu yote ya maji ili vinufaishe vizazi vijavyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live