Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upanuzi kituo kupoza umeme Bwawa la Mtera kukamilika Desemba

WhatsApp Image 2021 05 10 At 15.32.04.jpeg Upanuzi kituo kupoza umeme Bwawa la Mtera kukamilika Desemba

Tue, 11 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato, amesema hayo katika ziara ya kikazi kwenye kituo hicho cha kuzalisha umeme cha Mtera,ambacho uzalisha umeme Megawati 80 ambazo zinaingizwa katika grid ya taifa kwa ajili ya kupeleka umeme maeneo mbalimbali ya jijini Dodoma na Iringa.

Amesema, Gharama za Ujenzi wa mradi huo ni Sh. bilion saba,ambapo ujenzi wake ulisimama kutokana na sababu mbalimbali zilizonje ya uwezo wao lakini hivi sasa ujenzi huo utaendelea tena kwa kasi ili mradi huo wa REA awamu ya tatu uweze kukamilika.

“Nimekagua upanuzi wa mradi huu unaendelea vizuri,nimekagua pia mgodi na sehemu ya kutoa umeme, katika mitambo ambayo ina mapanga yanayozunguka kwa ajili ya kuzalisha umeme,” amesema Byabato.

Chanzo: ippmedia.com