Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uokoaji, kutafuta miili waliofariki Hanang waendelea

Hanang Hananggggg Uokoaji.jpeg Uokoaji, kutafuta miili waliofariki Hanang waendelea

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati uokoaji wa waathirika wa maporomoko ya tope kutoka Mlima Hanang zikiendelea, leo asubuhi hali ya hewa ilibadilika na mvua ilianza kunyesha tena.

Mvua hiyo ilianza majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumanne Desemba 5, ambapo iliendelea kupungua kuanzia saa mbili asubuhi leo.

Kukatika kwa mvua hiyo kulitoa nafasi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na vikosi vingine vya uokoaji kuendelea na shughuli ya uokoaji.

Aidha wananchi wameonekana wakiendelea kuokoa vitu mbalimbali katika nyumba zao na wengine katika sehemu za biashara.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa mji wa Katesh, Hanang na kutoa pole pamoja na kuongoza shughuli ya kuaga miili mingine, ambayo jana haikuweza kutambuliwa na ndugu zao kwa ajili ya taratibu zingine za maziko.

Mpaka sasa watu 63 wamepoteza maisha huku wengine zaidi wakihofiwa kufunikwa na tope.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live