Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unywaji pombe Kibondo watajwa kuwa kero

38418 Unywajipic Unywaji pombe Kibondo watajwa kuwa kero

Tue, 29 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibondo. Wananchi wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, wameziomba mamlaka za Serikali za vijiji na mitaa kutunga sheria kali ndogo kwa kila mwananchi atayebainika kunywa pombe kupita kiasi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema kumekuwapo na tatizo la baadhi ya wazazi na walezi kunywa pombe kupitiliza.

Mkazi wa Kibondo, Aisha Ramadhani amesema kuna baadhi ya watu kulewa kupindukia ni suala la kawaida.

Amesema pia kuna tabia ya baadhi ya wanawake kunywa  pombe kiasi cha kupoteza fahamu na wakati mwingine huokotwa miferejini wakiwa hawajitambui.

Aisha amesema hali hiyo husababisha watu kushindwa kutunza familia zao vizuri na kuchangia katika umaskini kwenye jamii. 

Tabia hiyo, kwa mujibu wa mkazi hiyo inachangiwa na mila zilizopo wilayani hapa ambapo watu kunywa pombe na kulewa kupita kiasi ni suala la kawaida.

Akizungumzia namna ya kukabiliana na suala hilo, mmoja wa wananchi waliojengewa uwezo na shirika lisilo la kiserikali la Kivulini, Nestol Ntibwela amesema wamekuwa wakiwaelimisha wananchi mara kwa mara ikiwa ni pamoja kuacha kukumbatia mila na desturi zinazomkandamiza mwanamke na mtoto.

"Kwa mila na desturi za watu wa Kigoma, mwanamke akipigwa na mumewe au mtoto kufanyiwa vitendo vya kikatili ni kitu cha kawaida na hakuna mtu anayeweza kwenda kutoa taarifa katika vyombo vya dola kwa hatua stahiki," amesema Ntibwela.

Akizungumza baada ya kutembelea jengo la dawati la jinsia wilayani humo lililojengwa na serikali chini ya Mpango wa Pamoja wa Kigoma (KJP), Balozi wa Norway nchini, Elisabeth Jocobsen amesema mkoa huo umekuwa ukipokea idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi za jirani lakini dhamira yao ni kuuimarisha mkoa huo.



Chanzo: mwananchi.co.tz