Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unamjua Trump wa Chato, huyu hapa

13952 CHATO+PIC TanzaniaWeb

Mon, 27 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Chato. Utakuwa unamjua Donald Trump Rais wa Marekani kutokana kuongoza Taifa hilo kubwa dunia, lakini yeye mwenyewe kuwa na vitega uchumi mbalimbali.

Kutokana na umaarufu huo wa Rais Trump, hapa nchini, mkazi wa kijiji cha Nyamirembe, wilaya ya Chato mkoani Geita, Bashiru Manampa amejipa jina la ‘Trump wa Chato.’

Jina hilo ameitwa kutokana na kumiliki vitega uchumi mbalimbali vinavyotoa ajira kwa wakazi wa Chato.

Miongoni mwa vitega uchumi hivyo ni kumiliki mifugo mingi na boti ndogo zaidi ya 10 zinazotumika katika uvuvi Ziwa Victoria zinazoendeshwa na vijana mbalimbali kwa ajili ya shughuli za kujiingiza kipato.

Trump wa Chato jana Agosti 26, 2018 alikutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba wakati alipotembelea kijiji hicho na kisiwa cha Magafu akiwa kwenye ziara yake ya kukagaua hali ya mazingira mkoani Geita.

Trump wa Chato ambaye shughuli zake zimekuwa zikifanyika katika kisiwa cha Magufu ambacho Waziri Makamba anataka kihifadhiwe, kigogo huyo wa Chato alimweleza waziri yupo tayari kuhamisha shughuli zake.

Si peke yake anayeishi kwenye kisiwa hicho kwa shughuli za uvuvi na ufugaji ambao kwa pamoja walikubali kuondoka.

Alisema ingawa alikuwa akiishi kisheria kisiwani humo lakini amechukua uamuzi ili kutii agizo la serikali ya wilaya iliyopendekeza kisiwa hicho kiwe ni miongoni mwa maeneo nyeti yanayopaswa kulindwa na kuhifadhiwa kwa kutumia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.

“Kile kisiwa kimezungukwa na mazalia ya samaki mheshimiwa waziri na wavuvi haramu wanakipenda, lakini tulivyoamua kuweka makazi kihalali tulifanikiwa kuwadhibiti waharibifu hawa wa mazingira na viumbe hao wa ziwani,” alisema Trump wa Chato.

“Tupo tayari kuondoka kama serikali ya wilaya iliavyoagiza ili Magafu ilindwe na kuhifadhiwa. Wasiwasi unaokuja ni kwamba Magafu ipo mbali je huo ulinzi utakuaje kwa sababu wanakijiji hawataruhusiwa kwenda tena eneo hilo kwa sababu litakuwa limetangazwa kisheria,” alihoji Trump wa Chato.

Alisema ameishi miaka mingi katika kisiwa hicho akifanya shughuli mbalimbali ikiwamo ufugaji wa mbuzi na kwamba hivi sasa yupo tayari kuondoka kama serikali ya wilaya ilivyoagiza ili Magafu ipate hadhi ya kulindwa kwa maslahi na maendeleo ya Chato.

Kwa upande wake, Makamba alielezea kufurahishwa namna wananchi wa Nyamirembe walivyoonyesha utayari na utashi wa kutaka kisiwa hicho kilindwe na kuhifadhiwa kwa maendeleo ya Chato.

“Nitatuma timu ya wataalamu kuja na kwenda katika kile kisiwa kwa ajili ya kuona na kutathmini namna tutakavyoweza kuanza mchakato wa kukilinda. Nimejionea namna kisiwa hicho kilivyokuwa na umuhimu kwenu kitakuwa kichocheo cha mapato kwa wilaya hii,” alisema Makamba.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz