Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy ataka uadilifu kwenye DNA

Ummy Pic Dna Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: Mwananchi

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameiagiza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa waadilifu kwenye kuchukua sampuli ya vipimo na kutoa majibu kwenye utaratibu wa kupima vinasaba binamu (DNA).

Ummy ameyasema hayo leo Jumamosi Februari 11 wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

“Kazi yenu inamahusiano makubwa na kwenda kutenda haki…Kwasababu mimi ni mwanamke na huwa navutwa sana na haki za wanawake, unakuta mwanaume kampa ujauzito mwanamke halafu anasema mimi sio mtoto wangu. Mtoto anazaliwa baba anakila kitu mtoto anahangaika,” amesema.

Amesema kuchunguza uhalali wa baba au mama ni yupi anaomba utumike uadilifu.

Amesema wataangalia namna nzuri ya ukusanyaji wa sampuli hizo kwasababu huwa zinakusanywa pia na Jeshi la Polisi na hospitali.

Ummy amewataka watu wanaotaka kupata huduma ya kufahamu wazazi halisi wa mtoto kufuata taratibu zilizowekwa ikiwa ni pamoja na kwenda ustawi wa jamii ambao watawapeleka mahakamani ili watoe kibali cha vipimo.

Ameiagiza mamlaka hiyo kutoa elimu kwa umma ni utaratibu gani watumie kufanya DNA ili kuepuka watoto wanaokataliwa na baba zao.

Naye Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Fedelice Mafumiko ujenzi huo unalenga katika kusogeza karibu huduma zinazotolewa na ofisi hiyo kwa Watanzania.

Amesema katika jengo hilo hilo litakuwa na maabara ya vinasaba vya binadamu ambalo wameipa kipaumbele kwa kuanza kuinunulia vifaa.

“Kutakuwa na maabara ya vinasaba vya wanyamapori, kemia, mikrobilolojia, bidhaa na uchunguzi wa mazao na mazingira na ofisi za watumishi na kumbi za mikutano,”amesema.

Amesema pia kwa huduma ya sayansi jinai, mashahidi wao wanaweza kutoa ushahidi kwa njia ya mikutano ya video.

Chanzo: Mwananchi