Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy ataja sababu kliniki ya kurekebisha maumbile kufanyika Tanga

Ummy Pic Ummy ataja sababu kliniki ya kurekebisha maumbile kufanyika Tanga

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo, itakuwa kituo cha umahiri wa upasuaji wa kurekebisha maumbile Tanzania na Afrika Mashariki.

Ummy ameeleza hayo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kambi ya upausaji wa kurekebisha maumbile iliyoanza Julai 14, 2023 inatekelezwa na Taasisi ya Interplast ya Ujerumani kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

Kupitia Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Chuo Kikuu cha afya na sayansi shirikishi muhimbili (Muhas) na Taasisi ya Mendeleo ya Tanga (Tadene).

Amesema upasuaji wa kurekebisha maumbile ni muhimu sana katika kuwarejesha watu waliopata ajali za kawaida, ajali za moto au uvimbe uwezo wa kufanya shughuli zao kama kawaida.

“Mwanzo walipokuja ofisini kunieleza juu ya kufanya kambi hii sikuelewa sana umuhimu lakini baada kupata hadithi ya kijana mmoja aitwaye Safari, aliyepata matatizo yaliyosababisha akatwe miguu hapa Bombo na kukaa na hali hiyo kwa miezi nane bila kutembea niliona umuhimu wa upasuaji huo,” amesema Waziri Ummy.

"Nilimkuta kijana huyo akiwa amelazwa Bombo na baadaye kuchukuliwa kupelekwa nchini Ujerumani ambapo amefanyiwa upasuaji na anaweza kutembea kama kawaida.

Nimelazimika kufanya mkutano huu nanyi waandishi baada ya kuulizwa maswali mengi kuhusu hii kambi na wengi wakidhani upasuaji huu ni ule wa urembo. “Watu wanasema upasuaji huu pengine ni wa Uturuki yamehamia Tanga.”

Akizungumzia kuhusu kuwekwa kituo hicho Bombo amesema ni kwasababu ya uhusiano uliopo kati ya Ujerumani na mkoa wa Tanga. Pia kuanzishwa kwa kituo hicho kutasaidia kueneza wataalamu watakaowapa mafunzo madaktari juu ya upasuaji wa kurekebisha maumbile.

Jumla ya watu 250 wamejiandikisha kwa ajili ya kupata huduma hiyo na upimaji wa awali umefanywa na waganga mahiri kutoka nchi ya Ujerumani Kwa mujibu wa kiongozi wa wataalamu hao kutoka ujerumani, Profesa Jurgen Dolderer amesema jumla ya watu 16 tayari wameshafanyiwa upasuaji huo ambao unaendelea hadi Julai 28 mwaka huu.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Japhet Simeo ameishukuru Taasisi ya Interplast ya Ujerumani na Wizara kwa kuleta huduma hiyo katika hospitali ya Bombo na kusema kuwa imewasaidia watu ambao kwa kawaida hawawezi kumudu gharama ya huduma hiyo ambayo kati ya milioni moja hadi mbili na zaidi.

Chanzo: Mwananchi