Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umeme warejea Kagera baada ya kukatika siku tatu

72460 Umeme+pic

Thu, 22 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati huduma ya umeme ikirejea katika mkoa wa Kagera, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema bado linaendelea kufanya juhudi ili kuhakikisha maeneo ya Muleba na Kanyigo mkoani humo yanapata huduma hiyo.

Mkoa wa Kagera ulikuwa gizani tangu Agosti 19, 2019 baada ya mti wa Caristus kuangukia nguzo za umeme mkubwa nchini Uganda na kukata waya katika njia ya umeme inayotoka Masaka kwenda Kagera Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tanesco jana Jumatano Agosti 21,2019 umeme ulirejea katika mkoa wa Kagera saa 2:40 usiku.

Kupitia taarifa iliyotolewa na shirika hilo, Agosti 20, 2019 inaelezea hitilafu hiyo ilisababisha Wilaya za Bukoba Mjini na Vijijini, Misenyi, Karagwe, Kyerwa na maeneo jirani kukosa huduma ya umeme.

“Wataalamu na mafundi walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha huduma ya umeme imerejea, ambapo viongozi waandamizi kutoka Tanzania na Naibu Kamishina wamekuwepo Masaka nchini Uganda kuhakikisha kazi hiyo inayofanywa na mafundi wa Uganda inakamilika na huduma ya umeme kurejea.” Inaeleza sehemu ya taarifa hiyo

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz