Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umeme warahisisha uzalishaji wa mayai Urambo

Mayai Ya Kisasa.jpeg Mayai

Sun, 24 Jul 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mmiliki wa shamba la mifugo la Mhanuka wilayani Urambo, Japhet Mhanuka ameeleza mbele ya Waziri wa Nishati, January Makamba namna ya mradi wa kupeleka umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ulivyomsaidia katika utekelezaji wa shughuli zake.

Shamba la Mnahuka lipo kijiji cha Yaleyale wilayani Urambo mkoani hapa lilianzishwa mwaka 2007 likiwa na miradi mbalimbali ikiwemo ya ufugaji wa kuku wa mayai, ngo' mbe wa kienyeji.

Japhet ameeleza hayo jana Jumamosi Julai 23, 2022 baada ya January kumtembelea katika eneo la kazi kuangalia shughuli zake hasa baada ya kupelekewa huduma ya umeme.Katika ziara hiyo January aliaambata na viongozi wa wilaya ya Urambo akiwemo mbunge wa jimbo hilo, Magreth Sitta.

Katika maelezo yake, Mhanuka amesema kabla ya huduma ya umeme walilazimika kuwa na matumizi makubwa ya kuni na mkaa kwa ajili moto unaozalisha joto linalotumika kwenye mabanda ya kuzalishia vifaranga vya kuku wa kisasa.Amesema hatua hiyo ilisababisha uzalishaji kuwa mdogo.

" Kulikuwa na changamoto ya kukosekana kwa mwanga wa kutosha kwenye mabanda, vifo vingi vya kuku hasa vifaranga vilikuwa vinatokea  hasa wakati wa baridi, hewa chafu kutokana na moshi wa mkaa.Hakukuwa na joto ka kutosha kwenye mabanda ya kuku.

" Lakini ujio wa umeme umeongeza uzalishaji  wa mayai kwa sababu kuna mwanga wa kutosha kwenye mabanda pamoja na joto.Pia uzalishaji wa kuku umeongezeka kutoka 200 hadi 8055,"  amesema Mnahuka.

Amesema ujio wa umeme Yaleyale umesaidia upatikana muhimu ya usindikaji wa unga kwa wanakijiji hao, akisema kwa sasa wanazalisha tani 100 za unga safi na bora.

Pia wamefanikiwa kufunga mashine  mbili za kukoboa  na kusaga sambamba na kutoa ajira kwa vijana 32 kwenye kuku, uzalishaji wa unga na ufugaji wa ng'ombe.

Daktari wa mifugo shamba hilo, Salome Bruno amesema kwa mwezi walikuwa wanatumia Sh700, 000 kwa ajili ya kununua magunia  ya mkaa pamoja na kuni kwa ajili ya shughuli hiyo, lakini sasa hivi kwa siku wanatumia unit nne za umeme.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz