Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umeme wakwamisha mshtakiwa kusomewa hukumu

81253 Kesi+pic Umeme wakwamisha mshtakiwa kusomewa hukumu

Tue, 22 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma imeahirisha kusoma hukumu ya kesi ya kuvunja nyumba  na kujeruhi inayomkabili mkazi wa Mkoa wa Kigoma, Hussein Rajabu (28).

Akiahirisha kesi hiyo leo Jumanne Oktoba 22, 2019 Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Kenneth Mutembei amesema ameshindwa kusoma hukumu hiyo kwa kuwa mahakamani hapo hakukuwa na umeme, hivyo kushindwa kuchapa nyaraka za hukumu.

“Hukumu ilipangwa kusomwa leo lakini ninaahirisha hadi Oktoba 29, ila mpaka leo jioni itakuwa imekamilika tayari kwa mshtakiwa

kusomewa hukumu yake,” amesema.

Katika kesi hiyo namba 57 ya mwaka 2019 inadaiwa Mei 20, 2019 eneo la Mwanga Vamia mshtakiwa alivunja nyumba usiku kwa nia ya kutenda kosa la kujeruhi na kosa la kujeruhi.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz