Ulinzi umeimarishwa leo Novemba 12 wakati kifimbo cha malkia wa Uingereza cha kuashiria uzinduzi wa michezo ya jumuiya ya madola kikiwasili Da es Salaam jioni hii.
Kifimbo hicho kilipokelewa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rick Shearn, Naibu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania.
Baada ya mapokezi hayo, kilipandishwa kwenye moja ya difenda za polisi iliyokuwa na askari wenye silaha na kuongozwa na king'ora kuelekea Centre Polisi, ambako kilikabidhiwa kwa OCD wa kituo cha Kati, Ilala, SSP Matride Kuyetu.
Kifimbo hicho kitalala kituo hapo hadi kesho saa 3:00 asubuhi kitakapopelekwa kituo cha Jakaya Kikwete ambako hafla ya kukimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Ikulu, Dar es Salaam.
Tanzania ni miongoni mwa mataifa 71 ambayo Kifimbo hicho chenye ujumbe wa Malkia kitakimbizwa kabla ya kuanza kwa michezo ya madola Julai 24 mwakani.
Timu za judo, ngumi, riadha, kuogelea na za michezo ya walemavi zimetajwa kuiwakilisha nchi kwenye michezo ya msimu huu.