Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulinzi waimarishwa Chato Magufuli akiagwa

Ulinziu Ulinzi waimarishwa Chato Magufuli akiagwa

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Rais Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam kwa ugonjwa wa moyo.

Katika uwanja wa Magufuli kuna mageti mawili yanayotumika na lile lililopo upande wa Kaskazini linatumiwa na viongozi Serikali na taasisi mbalimbali huku geti la upande wa pili likitumiwa na wananchi watakaoingia uwnajani kwa ajili ya kuaga.

Mapema alfajiri leo wananchi wameruhusiwa kuingia uwanjani huku vikosi vya ulinzi na usalama vikiimarisha ulinzi.

Kwa mujibu wa ratiba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atazungumza kabla ya kuanza shughuli ya kutoa heshima za mwisho kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni na mwili wa kiongozi huyo utarudishwa nyumbani kwake.

Hayati Magufuli atazikwa kesho katika kijiji cha Mlimani kilicho katika wilaya ya Chato Mkoani Geita.

Chanzo: ippmedia.com