Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukicheza na pesa za miradi nakufuta kazi - Bulembo

Untitled 1 (5) Ukicheza na pesa za miradi nakufuta kazi - Bulembo

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Halima Bulembo ametishia kuwaondoa kazini watendaji watakaofanya mchezo na shilingi milioni 180 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwajili ya ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023

Kauli hiyo ameitoa kwenye kikao cha kwanza cha robo ya kwanza cha baraza la madiwani katika mwaka wa fedha 2022/2023 katika Halmashauri ya wilaya ya Muheza

Bulembo ametoa angalizo juu ya matumizi ya kiasi cha shilingi milioni 180 fedha zilizotolewa na Rais kwajili ya ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa. 

"Huwezi kazi utasaidiwa yaani hatutogombana na mtu watu wanaotafuta kazi ni wengi sana kwahiyo kama kazi yako imeshakuwa ni mazoea unaweza kufanya unavyotaka tutakuja na tutakuambia kaa pembeni tutampa yule anayetaka hiyo kazi akusaidie huo ndio utaratibu wala hatutoshemeshana,"alisititiza Bulembo. 

"Ili tusifike huko mnaohusika mkasimamie inavyotakiwa tarehe 30 ndio dead line yangu mimi na viomgozi wa wilaya tutapokea hayo madarasa na tarehe 15 tutakuwa tunasubiria kumkabidhi Mkuu wa Mkoa na hapo hapo nitumie fursa hii kuwaambia watumishi wote na wakuu wa idara  kwamba kila mtu akafanye wajibu wake yaani hapa Muheza kuna mauzauza mengi yaani mtu tu akisikia ziara ya kiongozi ikipita anasema uuuuh Alhamdulillah mimi sijagswa  kwasabbau anajua angeguswa na yeye asingekuwa salama kwanini sasa tufikie huko, "alisema DC Bulembo. 

Katibu wa CCM Wilaya ya Muheza Saimon Leng'ese amempongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa namna alivyoshiriki kuibua matumizi mabaya ya fedha za miradi kwenye Halmashauro hiyo. 

"Tunashuhudia mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanyika hapa Muheza hata kama ilikuwa ni utamaduni uliozoeleka kule nyima lakini anayabeba na kuyafanyia kazi, "alibainisha Katibu huyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live