Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukeketaji mpya waibuka Kilimanjaro

UKEKETAJI 1 Ukeketaji mpya waibuka Kilimanjaro

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukeketaji mpya maarufu kwa jina la antena umeibuka mkoani Kilimanjaro ambapo hufanyiwa watoto wadogo.

Akizungumzia hali hiyo ambayo anadai imeibuka miongoni mwa jamii ya wakazi wa Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la GAESO mkoani humo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Hai, Happiness Eliufoo, amesema baadhi ya jamii wanaendeleza utamaduni huo uliopitwa na wakati na kusababisha vifo vya watoto na wengine kubaki na makovu ya kudumu.

"Wilaya ya Hai sio kisiwa; makabila yetu ya Wachaga, Wameru na Wamasai nao wanafanya ukeketaji na ukeketaji ulioko huku kwetu ni ule unaitwa antenna.

"Tunaiomba serikali yetu kupitia upya sheria ya ukeketaji na itoe adhabu kali ukiachana na hii adhabu ya sasa," amesema.

Amesema, jamii inakuja na mbinu mpya kila kukicha kuhusu ukeketaji na ikiwa hatua stahiki hazitachukuliwa kundi la watoto wa kike watafanyiwa ukatili wa kutisha, hivyo elimu inapaswa kuendelea kutolewa kwa jamii.

"Hapa kwetu mara nyingi kuna ukeketaji uliovuka kijiji, unakuta mtu anatoka Sanya Station anakwenda kukeketwa katika Kijiji cha Munge na zaidi tuko jirani na nchi ya Kenya, ambapo unakuta hizi jamii za kifugaji wanakwenda kukeketwa kule kwa wenzetu; hatupo salama tunahitaji elimu na mbinu zaidi ili kukomesha jambo hili,"amesema Happy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live