Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukatili wa kingono Kwimba na vikwazo vya kuudhibiti

F40296467aeec09c1c713965fbbe51e4 Ukatili wa kingono Kwimba na vikwazo vya kuudhibiti

Mon, 24 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MATUKIO 17 ya ukatili ukiwamo wa kingono kwa watoto yameripotiwa na kushughulikiwa katika o? si za wasaidizi wa kisheria wilayani Kwimba, Mwanza kati ya Mei na Juni mwaka huu.

Kati ya matukio hayo, matano ni ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto wa kike wenye umri chini ya miaka 18 na matukio 12 ni ya ukatili wa kimwili unaohusisha mashambulio kwa wanawake.

Mkurugenzi wa Shirika la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Kwimba, Mishano Sagalani, anasema katika mazungumzo na HabariLeo mjini Ngudu hivi karibuni kwamba, wasichana watano (majina tunayahifadhi) waliofanyiwa ukatili wa kingono ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

“Kati ya wasichana watano waliofanyiwa ukatili wa kingono, wanne kesi zao ziko polisi na mahakamani kwa hatua za kisheria,” anasema Sagalani.

Kuhusu wanawake 12 waliofanyiwa ukatili unaohusisha mashambulio ya mwili, Sagalani anasema ofisi yake imesaidia kusuluhisha 11 na moja inaendelea mahakamani.

Hata hivyo, anasema juhudi za kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake wilayani Kwimba zinakabiliwa na vikwazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya wananchi kutokuwa tayari kufichua matukio hayo.

“Vikwazo vingine ni waathirika na familia zao kutotoa ushirikiano wa kutosha katika vyombo vya kisheria dhidi ya watuhumiwa wa vitendo hivyo na uhasama unaojengwa na watuhumiwa dhidi ya wafichuaji wa uhalifu huo,” anaongeza.

Vikwazo vingine, kwa mujibu wa msaidizi huyo wa kisheria, ni baadhi ya viongozi wa vitongoji, mitaa na vijiji kugoma kutoa barua za kuwatambulisha waathirika wa ukatili katika vituo vya polisi, hali ambayo wakati mwingine kukataa kuwapokea waathirika hao wa ukatili.

“Pia wanajamii wengi wamekuwa wakiogopa kuripoti polisi vitendo vya ukatili kwa hofu ya kushikiliwa na kuunganishwa kwenye orodha ya mashahidi wa matukio hayo.

Kingine, tumebaini wanajamii wengi wana uelewa mdogo kuhusu matumizi ya Fomu Namba Tatu ya Polisi (PF 3) kama kiambatanisho muhimu cha ushahidi,” anaongeza Sagalani.

Kutokana na hali hiyo, Sagalani anasema elimu ya umuhimu na faida za matumizi ya fomu hiyo inahitajika kwa wananchi na viongozi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.

“Vilevile jamii ielimishwe faida za kujitokeza kutoa ushahidi na maofisa wa mashirika ya kupinga vitendo vya ukatili wapewe vyombo vya usafiri utakaowawezesha kufika maeneo ya matukio kwa wakati,” anaongeza.

Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini, Respectson Akyoo na Ofisa Mradi wa Boresha, Hamisi Kibayasi, wanasema ukatili wa kingono unatishia kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi ya kupata elimu, lakini pia unaweza kumfanya ashindwe kufikia ndoto yake.

Akyoo anasema ukatili wa kingono kwa watoto unachangiwa na uelewa duni wa wananchi kuhusu madhara ya vitendo hivyo, mila na desturi zisizozingatia usalama wa mtoto hali ambayo pia huchangia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) katika jamii. Mradi wa Boresha unatekelezwa chini ya Ushirikiano wa Kiimani Tanzania (The Tanzania Interfaith Partnership Association - TIP). Unaoundwa na taasisi nne za kidini ambazo ni Baraza la Wakristo Tanzania (CCT), Baraza la Kitaifa la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Baraza la Maaskofu Wakatoliki Tanzania (TEC) na Ofisi ya Mufti wa Zanzibar (MoZ). Maono ya TIP ni kutengeneza mtandao thabiti wa kiimani unaochangia uwepo wa jamii ya Kitanzania yenye afya na kizazi kisicho na Ukimwii.

Mkurugenzi wa Wasaidizi wa Kisheria, Sagalani na Mchungaji Mathias Mleka wa AICT Ngudu, Kwimba wanasema TIP imewapatia mafunzo ambayo yanawasaidia kuelimisha wananchi madhara ya vitendo vya ukatili ukiwamo wa kingono kwa watoto katika jamii.

“Tumegundua kwamba watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kingono katika sherehe na michezo ya ngoma… tunashukuru mafunzo tuliyopewa na TIP tunaendelea kuyasambaza na mwitikio wa jamii ni mkubwa,” anasema Mchungaji Mleka.

Kwa mujibu wa uta?ti kuhusu ukatili dhidi ya watoto ulifadhiliwa na UNICEF mwaka 2008 na kuratibiwa na timu ya wata? kutoka vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Altanta na Chuo Kikuu Shirikishi cha Afya na Sayansi ya Tiba.

Chanzo: habarileo.co.tz