Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukatili wa kimwili wakithiri kwa wanafunzi

9948d881febfe163ca2e3326b5ecffad Ukatili wa kimwili wakithiri kwa wanafunzi

Fri, 26 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

UKATILI wa kimwili dhidi ya wanafunzi, umetajwa kukithiri zaidi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari huku ukatili wa kingono ukifuatia.

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti inayohusu hali ya ukatili dhidi ya watoto wa shule Tanzania Bara, uliofanywa na Shirika la HakiElimu inaonesha kuwa asilimia 90 ya watoto wanafanyiwa ukatili wa kimwili.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dk John Kalage alisema utafiti huo ulifanyika mwaka jana na lengo kuu lilikuwa ni kupata taarifa rasmi na kujifunza hali halisi kuhusu ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto shuleni, na kuelewa vyanzo vya ukatili huo na kuboresha ulinzi na usalama wa watoto waliopo shuleni Tanzania Bara.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana na kushirikisha wadau mbali mbali wa elimu, inaonyesha kuwa watoto nje na ndani ya mazingira ya shule, wanafanyiwa matukio makubwa ya unyanyasaji katika mifumo tofauti.

Kalage alisema asilimia 87.9 ya watoto wote waliosailiwa katika utafiti huo uliofanyika kwa miezi sita kati ya mwaka 2019 na 2020, umebaini kukumbana na ukatili wa kimwili hususan kupitia adhabu za viboko.

Utafiti huo umebaini pia kuwa asilimia 17.0 ya watoto waliopo shule za umma na asilimia 14.3 waliopo shule binafsi, wamewahi kunyanyaswa kingono angalau mara moja wakati asilimia 34.3 ya watoto wa shule, wamenyanyaswa kisaikolojia hasa na wazazi au walezi.

Takwimu za Kituo cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC) zinaonesha uwepo wa kesi 24 zilizohusisha walimu watatu, kati yao wakiwa walimu wakuu, za unyanyasaji wa wanafunzi kingono.

Pia walimu 162 walifukuzwa kazi kati ya miaka ya 2016 na 2019 kwa kuhusika na matukio ya unyanyasaji wa kingono shuleni.

Chanzo: habarileo.co.tz