Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukarabati uwanja wa ndege Mwanza mbioni kuanza

11466 Ndege+pic TanzaniaWeb

Mon, 16 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) imesema taratibu kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza zimeanza.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumapili Julai 15, 2018 ofisa habari wa TAA, Mariam Lussewa amesema taratibu hizo ni maandalizi ya kuiwezesha ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner kutua katika uwanja huo.

Amesema nyaraka kwa ajili ya kuomba kufanyika kwa marekebisho hayo zimeshatumwa jijini Dar es Salaam na siku yoyote wiki ijayo, wakandarasi wataanza kazi.

Maboresho hayo ni ya njia za maegesho ya ndege pamoja na kituo cha hali ya hewa. Ndege hiyo yenye uwezo wa kupakia 262 itaanza kufanya safari zake Julai 29, 2018.

Kauli hiyo ya TAA imekuja zikiwa zimepita siku mbili tangu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kueleza kuwa ndege hiyo itaanza safari zake kati ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza na kuutaka uongozi wa uwanja wa ndege wa Mwanza kuanza marekebisho ili Dreamliner iweze kutua.

“Ni lazima tufanye marekebisho hayo haraka kwa sababu  kituo cha hali ya hewa kinatakiwa kujengwa katikati ya uwanja hivyo wakandarasi wafanye haraka,” amesema Kamwelwe.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz