Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukarabati uwanja wa ndege Mtwara wafikia asilimia 85

Uwanja Wa Ndege Mtwara Ukarabati uwanja wa ndege Mtwara wafikia asilimia 85

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mtwara unaogharimu kiasi cha Sh55.2 billioni umefikia asilimia 85.

Mhandisi mshauri anaesimamia kitengo cha ushauri wa kihandisi kutoka wakala wa barabara nchini, (Tanroads), Dotto John amesema kuwa ukarabati wa kiwanja hicho unatarajiwa kukamilika Januari 31, 2022.

Amesema kuwa ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho unahusisha kupanua njia ya kurukia na kutua ndege kutoka upana wa mita 30 za sasa hadi mita 45 na kujenga upya matabaka ya barabara ya kurukia na kutua ndege.

Amefafanua kwamba pia kuongeza urefu wa barabara ya kurukia na kutua ndege kutoka mita 2258 hadi mita 2800.

Uboreshaji wa kiwanja hicho pia utahusisha kujenga maegesho mapya ya ndege katika eneo jipya kulingana na mpango kabambe (master plan) na kujenga barabara mpya ya magari ya kuingia kiwanjani pamoja na maegesho ya magari.

"Ukarabati na upanuzi wa kiwanja hiki pia unahusisha kujenga na kuimarisha maeneo ya usalama kiwanjani na kuweka vifaa vya zimamoto na kujenga tanki la kuhifadhi maji yenye uwezo wa kuchukua mita za ujazo 200.

Advertisement Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema kuwa kiwanja hicho kitakapokamilika kitakua miongoni mwa viwanja vitano vikubwa nchini na bora barani Afrika.

Amesema kuwa kitakua na uwezo wa kubeba ndege kubwa za abiria na mizigo kitakapokamilika upanuzi wake uliopo kwenye mpango mkuu.

Mkandarasi aliyeshinda zabuni za mradi huo ni kampuni ya kichina ijulikanayo kama Beijing Construction engineering group company limited kwa gharama za Sh 55.2 billioni.

Meneja mradi wa kampuni hiyo ya kichina,  Cui Ruitao ameiambia Mwananchi leo Jumatano Desemba 29 kuwa pamoja na changamoto ya  upatikanaji wa kokoto zinazopatikana eneo la Chipite umbali wa zaidi ya kilometa 140 kutoka eneo la mradi inayotokana na kuchelewa kwa malipo wao wameamua kulipia kokoto hizo ili mradi uendelee.

"Tunazo kokoto za kutosha kuendelea na kazi tumetoa pesa zetu tumeilipa kamouni ya kilebanoni ambao ndio wanatusambazia kokoto" amesema Ruitao

Katika taarifa za mradi ilitarajiwa kokoto hizo kupatikana katika eneo la Mtegu tofauti na uhalisia.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz