Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukarabati MV Magogoni kugharimu bilioni 7.5/=

Magogoni Mv Ukarabatiii Ukarabati MV Magogoni kugharimu bilioni 7.5/=

Thu, 16 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema, ukarabati wa Kivuko cha MV Magogoni ni juhudi na mikakati ya serikali katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji nchini.

Amesema ukarabati wa kivuko hicho utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 7.5, gharama ambazo ni pamoja na kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Profesa Mbarawa amesema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ukarabati wa kivuko hicho katika viwanja vya Kivukoni jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa miradi mitano ya ujenzi wa vivuko vingine vipya na miradi 16 ya ukarabati wa vivuko unaendela hivi sasa nchini, baada ya kusainiwa kwa mikataba yake ambayo hadi kukamilika kwa miradi hiyo itagharimu shilingi bilioni 60.7.

Profesa Mbarawa amewataka watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kusimamia vema ukarabati wa kivuko hicho utakaofanyika Mombasa nchini Kenya chini ya kampuni ya African Marine and General Engineering Company Ltd kwa muda wa miezi mitano.

Kivuko cha MV Magogoni kilijengwa mwaka 2008, kina uwezo wa kubeba abiria elfu mbili na tani 500 za mizigo yakiwemo magari madogo 60 kwa wakati mmoja.

Kina urefu wa mita 72.5, upana wa mita 17.4 na kina cha kuelea (draft) mita 1.7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live