Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukame wasababisha Ndama kunyweshwa uji badala ya maziwa

HHHHHHHHHHHHH Ukame wasababisha Ndama kunyweshwa uji badala ya maziwa

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafugaji wa jamii ya Kimaasai waliopo Chalinze, Kata ya Ubena mkoani Pwani, wanalazimika kuwanywesha uji Ndama (Mtoto wa Ng'ombe) wao kufuatia maeneo wanayotumia kulishia mifugo kukumbwa na hali ya ukame na kusababisha ng’ombe kushindwa kutoa maziwa.

Wafugaji hao wamesema kwamba hali iliyopo sasa ni ngumu kwao, kwani ukame umewaathiri na kupelekea baadhi ya mifugo kufa, huku wengi wakijitahidi kuwanusuru kwa kuwalisha pumba.

Kwa mujibu wa taarifa ya WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo, imeeleza kuwa nchi inakabiliwa na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, na kwamba baadhi ya matatizo yameanza kujitokeza ikiwamo vifo vya wanyama.

Waziri Jafo amesema hali ya ukame inashamiri kila mahali na wameendelea kupata taarifa kwenye baadhi ya mikoa, ng'ombe na mbuzi wanaendelea kufa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live