Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi wa daraja jipya la Simiyu wanukia

WhatsApp Image 2021 12 18 At 11.08.13 1080x640.jpeg Ujenzi wa daraja jipya la Simiyu wanukia

Sat, 18 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema ipo mbioni kuanza kumtafuta mkandarasi atayekejenga Daraja jipya la Simiyu lililopo katika barabara kuu ya Mwanza – Musoma lenye urefu wa mita 139.92 na upana wa mita 3 ambalo limedumu takribani miaka 67 toka kujengwa kwake.

Amesema hayo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, wakati akilikagua daraja hilo lililopo Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza na kuunganisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Arusha na nchi jirani ya Kenya na kusisitiza kuwa fedha tayari zimeshatengwa.

“Serikali imeamua kujenga Daraja hili lililojengwa toka mwaka 1954 ambapo sasa limechoka na hivyo Serikali imeitengea bajeti kwa mwaka huu wa fedha 2021/22 na kazi inayofata ni kuitangaza kupata mkandarasi na kulijenga upya na la kisasa”, Amesema Prof. Mbarawa.

Aidha amewatoa hofu wananchi wote wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani ambao wanatumia daraja hilo kusafirisha abiria na mazao sasa kilio chao kimesikika na daraja linaenda kujengwa na fedha zipo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, amemueleza Waziri huyo umuhimu wa daraja hilo kukamilika kujengwa mapema kwani lina watumiaji wengi ambao ni wakulima, wavuvi, wafanyabiashara wanaosafirisha mazao yao kutoka eneo moja hadi jingine.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Mwaza, Mhandisi Boniface Mkumbo, ameeleza kuwa Daraja hilo litajengwa kisasa na litakuwa na uwezo wa kuruhusu magari mawili kupishana na sehemu za watembea kwa miguu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live