Mwanza. Ujenzi wa chelezo na meli mpya katika ziwa Victoria unaofanyika katika bandari Bandari ya Mwanza Kusini imekamilika kwa asilimia 30.
Ofisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL), Erick Hamissi amesema ujenzi wa meli hiyo itakayosafirisha abiria 1, 200 na tani 400 ya mizigo kati ya bandari ya Bukoba na Mwanza umekamilika katika hatua ya michoro, kuagiza vifaa na ukataji wa vyuma.
Akizungumza na Waandishi wa habari katika ziara ya kukagua kazi hiyo leo Mei 20, 2019, Hamissi amesema tayari Serikali imelipa asilimia 35 ya Sh89 bilioni za kutekeleza mradi huo kwa kampuni ya Gas Enter ya Korea Kusaini.
Hafla ya kutia saini mkataba wa ujenzi wa chelezo na meli hiyo ulioshuhudiwa na Rais John Magufuli jijini Mwanza Septemba 2, 2018.
Kaimu mhandisi Mkuu wa MSCL, Abel Gwamafyo amesema ujenzi wa chelezo itakayotumika kujenga meli hiyo na nyingine zitakazojengwa baadaye tayari umekamilika kwa asilimia 30.
“Ujenzi wa chelezo kwa gharama ya Sh36 bilioni ulioanza Februari mwaka huu unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja,” amesema Gwamafyo.
Pia Soma
- HakiElimu yazoa tuzo Afrika
- Tuhuma 157 za rushwa zapokelewa Zanzibar
- Serikali ya Tanzania yaeleza mkakati wake kuhamasisha ufugaji nyuki
- Polisi kumpa dhamana kiongozi wa Chadema
Usafiri wa majini kati ya miji hiyo miwili ya mikoa ya Kanda ya Ziwa umekuwa wa kusuasua tangu kuzama kwa meli ya Mv Bukoba mwaka 1996, uchakavu na kuharibika kwa meli za Mv Victoria na Mv Serengeti zilizositisha huduma kati ya mwaka 2014 na 2015.