Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi wa barabara kufungua fursa Mafia

Bashungwa Awasili Morogoro, Atekeleza Agizo La Rais Samia Kufika Pasipofikika Ujenzi wa barabara kufungua fursa Mafia

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuifungua wilaya ya Mafia kwa kujenga miundombinu bora ya barabara ili kuchochea fursa za kiuchumi, Utalii na Uwekezaji. - Bashungwa amesema hayo katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wananchi wa Kirongwe Wilayani Mafia katika ziara yake ya Kikazi ya kukagua hali ya miundombinu ya barabara pamoja na utendaji wa Kivuko cha MV Kilindoni kinachotoa huduma kati ya Nyamisati – Mafia. - Bashungwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Wizara ya Ujenzi kuanza taratibu za kumpata Mkandarasi atakayejenga barabara ya Kilindoni – Rasmkumbi (km 52.28) kipande kilichobakia cha kilometa 50 kwa kiwango cha lami baada ya kukamilisha ujenzi wa kipande cha Kilindoni – Kigamboni (km 2.1) - Aidha, Bashungwa amemuelekeza Meneja wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Pwani kuikarabati barabara ya kutoka Bungu hadi Nyamisati (km 40) kwa kiwango cha changarawe ili iweze kupitika wakati wa mvua na kiangazi. - Naye, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambaye pia nia Mbunge jimbo la Mafia, Omary Kipanga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kukiona kisiwa cha Mafia na kuleta fedha za miradi mbalimbali ambazo zimeboresha huduma kwa wananchi wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live