Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana amesema ujenzi wa stendi mpya wa mabasi ya mkoani ya Mbezi Luis umefikia asilimia 20 hadi sasa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Ujenzi huo kwa sasa upo ngazi ya msingi unatekelezwa eneo la Mbezi Luis ulianza Januari 2019 changamoto hiyo imesababisha mkandarasi anayejenga stendi Hainan International kushindwa kutoa baadhi ya vifaa vyake vya ujenzi bandarini, hali inayochangia ujenzi huo kutokwenda na wakati.
Stendi hiyo mpya ambayo itatumiwa na mabasi ya kwenda mikoani na nje ya nchi itagharimu Sh50.9 bilioni ikijumuisha na ujenzi wa maduka makubwa, mabenki na itakuwa na huduma mbalimbali za kijamii
Sipora ameeleza haya leo Ijumaa, Juni 21, 2019 mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi huo.
“Mheshimiwa waziri suala la VAT nimelifuatilia sana ikiwemo kwenda Hazina Dodoma, hadi sasa sijafanikiwa. Wiki iliyopita niliambiwa kuwa kamati imeshakaa na kuidhinisha, kilichobaki waziri atoe idhini kwa (AG) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye atatangaza (GN) katika gazeti la Serikali. Hii ndio hatua iliyobaki.”
“Kuna vitu vingi vimekwama pale bandarini na kazi ingeweza kwenda mbali zaidi, licha ya kujitahidi. Tuna wasiwasi tukimruhusu mkandarasi anunue vitu ili baadaye arudishiwe fedha itakuwa mtihani,” amesema Liana.
Pia Soma
- Shule ya Kifaransa yatoa fursa kwa Watanzania
- Serikali yafungua mnada wa kimataifa wa mifugo Longido
- Jaji Mkuu Zanzibar awapa somo majaji, mahakimu
- VIDEO: Bwana harusi aanguka wakati wa kumuaga bibi harusi aliyekufa ajalini Mbeya
Kuhusu VAT, Jafo amesema “Ile message (ujumbe) ulionitumia siku mkurugenzi niliupeleka moja kwa moja kwa Dk Mpango (Philip -Waziri wa Fedha na Mipango), nilimwambia watu wangu wa Ubungo wamekwama katika VAT. Siyo mradi huu ipo mingi ikiwemo ya Benki ya Dunia, lakini nina imani atalifanyia kaz.”