Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi mwendokasi Mbagala wafika asilimia 82

Mbagala Mwendokasi Ujenzi mwendokasi Mbagala wafika asilimia 82

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema Awamu ya Pili (BRT II) ya ujenzi inayohusisha barabara ya Kilwa kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea Mbagala na barabara ya Kawawa kutoka makutano ya Magomeni kupitia Chang’ombe hadi makutano ya barabara ya Kilwa umefikia asilimia 82.

Hayo yamesemwa bungeni na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

“Mradi huu una barabara zenye urefu wa kilomita 20.3; vituo vya mabasi 29; Barabara za juu mbili; majengo mawili ya Terminal; Depot moja na Feeder station nne

“Aidha, Awamu ya Tatu (BRT III) inayohusisha Barabara ya Nyerere kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam hadi Gongolamboto yenye urefu wa kilomita 23.6 imekamilika kwa asilimia 5,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live