Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi mwendokasi Gerezani-Mbagala kukamilika Aprili

Mwendokasipic Ujenzi mwendokasi Gerezani-Mbagala kukamilika Aprili

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema awamu ya pili ya ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka kutoka Gerezani hadi Mbagala Rangi tatu, utakamilika Aprili.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 20.3. Pia ujenzi wa vituo 27 vya mabasi ya mwendo wa haraka, barabara za juu tatu na njia za maji za chini zenye urefu wa kilomita 40.

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Febuari 27, 2023 wakati akikagua ujenzi wa awamu ya tatu ya barabara ya mabasi yaendayo haraka kutoka Gerezani hadi Gongo la Mboto yenye urefu wa kilomita 23.3 utakaogharimu Sh 231 bilioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live