Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi chuo cha Veta wakwama kwa miezi 10

Be3336cf5f413a945482a66026e1cdc4 Ujenzi chuo cha Veta wakwama kwa miezi 10

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UJENZI wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, umesimama kwa zaidi ya miezi kumi huku Mkandarasi Kampuni ya Kichina ya Tender International Co Ltd ameshalipwa Sh bilioni 3.7.

Hii ni baada ya serikali kusimamisha mkataba wa ujenzi baada ya mkandarasi huyo kusuasua katika utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya Sh bilioni10.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mkoani Mbeya, Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Shomari Chololo alikiri kusimama kwa ujenzi wa mradi huo uliokuwa ukitekelezwa mjini Sumbawanga tangu Januari mwaka huu.

Akifafanua alisema kiasi kikubwa kusuasua kwa mradi huo umesababishwa na sintofahamu iliyojitokeza kati ya mkandarasi na Veta Makao Makuu.

"Si unakumbuka tangu kipindi kile alipokuja aliyekuwa Waziri wa Elimu (Profesa Joyce Ndalichako) na kubaini mapungufu kadhaa ya kimkataba .... mkandarasi aliondolewa hadi sasa, lakini tuna uhakika kazi itaanza tena hivi karibuni kwani kuna mipangosSerikali inaweka sawa," alisema Chololo.

Aliongeza kusema utekelezaji wa mradi huo ulianza Julai 31, mwaka 2018 ukitarajiwa kumalizika Septemba mwaka jana kwa gharama ya Sh billioni 10.7.

"Fedha hizo ni mkopo kutoka African Development Bank (ADB), hadi mkandarasi anasitishwa kuendelea na kazi alikuwa amelipwa zaidi ya Sh billioni 3.7," alifafanua.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na HabariLEO walidai athari za kuvunjwa kwa mkataba huo zimewagusa moja kwa moja wananchi wa Sumbawanga na mkoa wa Rukwa kwa kuwa kama mkandarasi angemaliza kwa wakati kazi ya ujenzi wa chuo hicho kingekuwa kimeanza kuchukua wanafunzi wa masomo ya ufundi stadi.

Chanzo: habarileo.co.tz