Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi barabara mwendokasi Mbagala wafikia asilimia 44

Mbagala Mwendokasi Ujenzi barabara mwendokasi Mbagala wafikia asilimia 44

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji Mkuu Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Dk Edwin Mhende amesema mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mabasi hayo kwenda Mbagala umefikia asilimia 44.4%.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dk Mhende amesema mradi huo unatarajiwa kukamilishwa Machi, 2023 kama mkataba unavyoeleza.

"Kwa upande wa Mbagala hadi sasa ninapozungumza asilimia 44.4 wa ujenzi wa miundombinu wezeshezi itakayotufanya sisi tupeleke huduma hii ya mwendo kasi kule imekwisha, ninapozungumza  na mkandarasi atakamilisha mwezi Machi mwaka ujao” amesema.

Awali mkufunzi wa mafunzo hayo KAIZEN, Jane Lyatuu kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara amesema wanatoa mafunzo hayo kwa lengo la kuboresha falsafa ya ubora na tija ili viwanda kuwa bora.

Naye, Meneja Mpangaji Ratiba na Udhibiti kutoka Kampuni ya Usafiri wa Mfumo wa Mabasi hayo,  Daniel  Madilu amesema huduma za usafiri huo zinafika hadi Mjini Kibaha.

Amesema kuwa mafunzo hayo yamempa uwezo wa kujua matarajio makubwa kutoka kwa wateja na namna ya kuboresha huduma hizo.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live