Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi Bwawa la Kidunda kumaliza kero ya maji DSM, Pwani

Bwawa Kidundaaaaaaa.png Ujenzi Bwawa la Kidunda kumaliza kero ya maji DSM, Pwani

Wed, 1 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda unaotarajiwa kuanza hivi karibuni mkoani Morogoro utagharimu Sh bilioni 346. Unatekelezwa na serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), unatarajia kuanza mwaka huu na kukamilisha mwaka 2026.

Ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita bilioni 190 na utakuwa suluhu ya tatizo la upungufu wa maji mkoani Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (RC), Fatma Mwassa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja alisema mradi utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu.

Alisema kukamilika kwake kutamaliza changamoto ya upatikanaji wa maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. “Tumekuja kuomba ushirikiano na uongozi wa mkoa katika usimamizi wa mradi huu ikiwa ni pamoja na ulinzi wa watu na miundombinu ambayo itawekwa,” alisema Luhemeja.

Alisema mradi huu wa kimkakati utahitaji ulinzi wa miundombinu yake ili utekelezwe ndani ya muda uliokusudiwa. Luhemeja alisema shughuli mbalimbali zimekwishafanyika kuelekea utekelezaji wa mradi huo ikiwamo ulipaji wa fidia kwa wananchi waliopisha mradi, ujenzi wa huduma muhimu za kijamii kama vile shule na kituo cha afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live