Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uharibifu mazingira wahatarisha upatikanaji maji Mtwara

Mazingira Majiiiiii Uharibifu mazingira wahatarisha upatikanaji maji Mtwara

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahitaji ya maji kwa mji wa Nanyamba ni lita 2,000,000 lakini tunazalisha lita 500,000 kutoka kwenye visima vitatu.

Hata hivyo viwili ni vibovu na tuko katika maboresho vikikamilika tunaweza kuongeza lita 15,000 kwa saa ambapo kwa siku tutapata lita 400,000 ili kupunguza tatizo la wananchi kukaa na kusubiri maji kwa muda mrefu. Akizungumza baada ya kutembelea chanzo hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara (Mtuwasa), Mhandisi Rejea Ng’ondya alisema kuwa licha ya uwepo wa uhaba wa maji lakini shughuli za kibinadamu zinaweka visima hivyo kwenye mazingira hatarishi. “Pamoja na hatua tunazochukua za maboresho lazima tuwe makini na utunzaji wa maji katika vyanzo vyetu ulimaji katika eneo hili unahatarisha kiwango cha maji kinachoweza kupatikana hapa ambapo tupo katika hatua za kufufua visima visivyofanya kazi na kuongeza vingine zaidi,” amesema.

“Kwa ushauri wangu visima vya aina hii tunatamani shughuli za kibinadamu ziweze kufanyika umbali wa zaidi ya mita mia tano kutoka kwenye visima kwa kuwa mita sitini ni sheria ya mazingira kutoka kwenye kingo za mito na hii siyo mito ndio maana na sisi tunashauri iwe hivyo ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi wetu,” amesema.

Meneja wa Kanda ya Nanyamba Mji, Leonard Ngingo alisema kuwa eneo hilo lina visima 5 ambapo kisima kikubwa kinazalisha lita 10,000 za maji kwa saa na kingine kinazalisha lita 8,000 za maji kwa saa.

“Kisima kina uwezo wa lita 8,000 kwa saa ingawa kwa sasa hakifanyi kazi na mikakati ya kukifufua inaanza yawezekana tukifufua tusipate kiwango tarajiwa kutokana na uharibifu wa mazingira uliofanyika karibu na chanzo hicho cha maji,” amesema Ngingo.

Mkazi wa Mnyawi Nanyamba, Kisura Nambingu alisema kuwa wapo watu wanashiriki kuharibu vyanzo vya maji hapa na wengine miundombinu elimu itolewe ili kutupunguzia hali ngumu ya upatikanaji wa maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live