Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhalifu wapungua kwa asilimia 18.2 pwani

8866a8ec63b89db74efba7a8fd62c7fe Uhalifu wapungua kwa asilimia 18.2 pwani

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

UHALIFU mkoa wa Pwani umepungua kwa asilimia 18.2

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema jeshi hilo limeweza kudhibiti vitendo vya uhalifu kutoka matukio 2,189 mwaka 2019 hadi matukio 1,791 mwaka 2020 na kusema hali hiyo ni sawa na upungufu wa matukio 398 au asilimia 18.2.

Aidha makosa dhidi ya binadamu yaani mauaji, ubakaji, wizi wa watoto na usafirishaji haramu wa binadamu.

yamepungua kutoka makosa 377 kwa mwaka 2019 hadi matukio 367 kwa mwaka 2020 ikiwa ni upungufu wa matukio 10.

Kamanda Nyigesa alisema hali hiyo imesababishwa na ushirikiano uliopo kati ya jeshi hilo na wananchi.

Nyigesa alisema kwenye makosa ya kuwania mali kama vile unyanganyi wa kutumia silaha, unyanganyi wa kutumia nguvu, uvunjaji, wizi wa pikipiki, wizi wa mifugo, na wizi wa magari yamepungua kutoka makosa 1,058 mwaka 2019 hadi 735 mwaka 2020 ambapo ni upungufu wa matukio 323.

"Kwenye makosa ya maadili ikiwa ni pamoja na kupatikana na silaha, utumiaji na uvutaji wa bangi,dawa za kulevya viwandani, kupatikana na pombe ya moshi na mitambo yake yamepungua kutoka makosa 754 mwaka 2019 hadi makosa 689 kwa mwaka 2020,"alisema Nyigesa.

Alisema kuwa kwa upande wa ajali za barabarani zimepungua kutoka 64 mwaka 2019 hadi 57 mwaka 2020 tofauti ya ajali saba sawa na asilimia 11 zilizotokea.

"Kwa upande wa wahamiaji haramu walikamatwa 332 ambapo kutoka Ethiopia walikuwa 326, Somalia mmoja, Congo watatu, Burundi mmoja na Rwanda mmoja ambapo walichukuliwa hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kurudishwa makwao,"alisema Nyigesa.

Alibainisha kuwa pia walifanikiwa kukamata madumu ya mafuta ya kupikia 2,139 ambayo yalikwepa kulipiwa ushuru aina ya Mico Gold ambayo yalikuwa na jumla ya lita 42,780 huku watuhumiwa 38 wa kukwepa ushuru wakiwa wamefikishwa mahakamani.

"Katika uhujumu uchumi jeshi limefanikiwa kukamata nyara za serikali zenye uzito wa kilogramu 350 zikiwa na thamani ya shilingi milioni 253.5 pamoja na pikipiki moja iliyotumika kusafirishia nyara hizo,"alisema Nyigesa.

Chanzo: habarileo.co.tz