Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhaba wa vitanda wawalazimu wanafunzi kulala chini

Uhaba wa vitanda wawalazimu wanafunzi kulala chini

Tue, 12 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mpwapwa. Wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari ya Chunyu Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma wanalazimika kulala chini kutokana na mabweni yao kukosa vitanda.

Hayo yamebainika leo Jumanne Machi 12, 2019 baada ya wanawake wa  Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwenda kuwasha umeme katika shule hiyo.

Wanawake hao wamegharamikia gharama zote za uingizwaji umeme katika shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo yalifanyika kimataifa Machi 8, 1019.

Tumaini Tarimo ambaye ni mwanafunzi katika shule hiyo amesema wanalazimika kutandika magodoro chini kwa kuwa hakuna kitanda hata kimoja katika mabweni hayo ambayo wanayatumia kulala wanafunzi wanaotoka mbali.

“Tunawaomba wadau wa elimu kutuangalia kwa sababu hata idadi ya wanafunzi tunaolala kwenye mabweni hayo ni kubwa kwa sababu idadi inayotakiwa ni wanafunzi wanne kwa kila chumba lakini tunalazimika kulala wanafunzi kati ya nane hadi kumi,” amesema Tarimo.

“Msongamano huo wa wanafunzi unatokana na kutokuwa na vitanda katika mabweni hayo kwa sababu kama vingekuwepo kila chumba kingekuwa na idadi sawa ya wanafunzi wanaohitajika kulala humo,” ameongeza

Agnes Mwaluko amesema msongamano wa wanafunzi kwenye mabweni umesababishwa na kutokuwa na miundombinu inayotakiwa kwenye mabweni

hayo kwani mabweni hayo yalijengwa kwa ajili ya wanafunzi 48 kila moja

lakini idadi ya wanafunzi wanaolala humo inazidi.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa Tanesco, mwenyekiti wa wanawake

hao, Renilda Kageuka amesema uamuzi wa kugharamia uingizwaji wa umeme

kwenye shule hiyo ni kuwafanya wanafunzi hao kusoma kwa bidii bila

vikwazo vya ukosefu wa nishati ya umeme.

Sambamba na hilo wanawake hao wametoa msaada wa vitabu vya masomo

mbalimbali vyenye thamani ya Sh1 milioni katika shule hiyo ili

kuwawezesha wanafunzi hao kuwa na vitabu vya kutosha kwa ajili ya

kujisomea.

“Tumewaletea umeme hapa shuleni kwenu ili msiwe na sababu ya kufanya vibaya kwenye masomo yenu hasa kwenye mitihani yenu ya kitaifa, itumieni nafasi hii ili muweze kutimiza ndoto zenu mlizojiwekea,” amesema Kageuka



Chanzo: mwananchi.co.tz