Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufaulu wa mitihani waongezeka mfululizo Dodoma

Ufaulupic Data Ufaulu wa mitihani waongezeka mfululizo Dodoma

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Ufaulu wa mitihani ya kuhitimu darasa la saba (PLSE) umeongezeka katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania kutoka asilimia 76.19 kwa mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 83.34 mwaka 2021.

Akizungumza katika kikao cha ushauri cha Mkoa (RCC), Ofisa Elimu Taaluma mkoani hapo, Abdallah Migila amesema ukilinganisha na mikoa iliyoshika nafasi 10 juu kitaifa, Dodoma umeachwa kwa asilimia ndogo.

Migila amesema mkoa wa Pwani ambao umeshika nafasi ya 10 juu kwa ufaulu kitaifa umeupita Mkoa wa Dodoma kwa asilimia 1.18.

Pia amesema ufaulu wa mitihani hiyo umeongezeka katika halmashauri za wilaya zote ukilinganisha na mwaka 2020.

“Halmashauri za Bahi, Chemba na Kondoa Mji zimetambuliwa na Baraza la Mitihani Nchini kuwa ni miongoni mwa halmashauri 10 kitaifa zenye ongezeko la ufaulu kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo,”amesema.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk Fatuma Mganga amesema kuwa miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na mkoa katika kuongeza ufaulu ni kuwawawezesha wanafunzi hao kufanya mitihani ya mara kwa mara kabla ya kufanya mtihani wa Taifa.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz