Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufaulishaji wa mafuta watajwa chanzo mlipuko wa moto kigamboni

Moto Ufaulishaji Mafuta Ufaulishaji wa mafuta watajwa chanzo mlipuko wa moto kigamboni

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Ajali ya moto iliyoteketeza malori mawili ya mafuta eneo la Kigamboni jijini hapa umedaiwa kusababishwa na ufaulishaji wa mafuta.

Wakizungumza katika eneo hilo leo Oktoba 7, baadhi ya magari yaliyokuwepo eneo la tukio wamesema, mlinzi wa kituo cha mafuta eneo la Sahara kulipotokea ajali anafahamu kila kitu.

"Hili jenereta si la kampuni, walileta hapa kufaulisha mafuta, hizi nyaya ni za bomba ambalo lilitumika kutoa mafuta kwenye gari, kuna gari lilikuwa jirani hapa nalo lilishika moto wakakimbia kulizima huko mbele," amesema dereva mmoja ambayo hakutaka kutajwa jina lake.

Kwenye ajali hiyo iliyotokea usiku majira ya saa tano usiku, madereva hao wamesema hakukuwa na shida yeyote kwenye magari hayo.

“Mimi niliondoka kwenda kubadilisha tisheti, uliponiaga kwenda msikitini muda mfupi napigiwa simu njoo moto unawaka, nimekuja nikamkuta mwanajeshi yupo na mtungi wa kuzima moto nikamuomba nitoe gari langu.

Madereva wenzangu wengi walifukuzwa walipaki magari hapa, lakini yalikuwepo magari matatu pembezoni mwa kituo cha mafuta malori mawili na gari dogo moja jeusi," ameeleza dereva huyo.

Hata hivyo, akizungumza kwa njia simu, Mkuu wa Wilaya ya Kigambon Fatma Nyangasa ametaka wataalamu waachiwe kazi yao kuchunguza suala hilo.

"Tuna wataalamu tumewapa hiyo kazi, wanajua wafanye nini na wanafanya utaratibu gani, tuwape nafasi wafanye kazi yao tusiwapotoshe watu.

“Jana kila mtu anasema matanki yanalipuka mara kituo cha mafuta jeshi watakuja na taarifa kamili," amesema Nyangasa.

Chanzo: mwanachidigital