Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Udom waanzisha programu mbili mpya

67075 UDOM+PIC

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom),  Profesa Faustine Bee amesema chuo hicho kitaanza kutoa shahada ya kwanza ya lishe tiba na chakula na shahada ya pili ya matibabu ya afya katika mwaka wa masomo 2019.

Ameyasema hayo leo Jumanne Juni 16, 2019 katika maonyesho ya vyuo vikuu nchini yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Profesa Bee amesema kuanzishwa kwa shahada ya masuala ya lishe na chakula kunakifanya chuo hicho  kuwa cha kwanza nchini kufundisha masomo hayo.

“Ni jambo jema kwa sababu lishe inatusaidia kutuweka katika hali nzuri, ni ya kwanza nchini japokuwa chuo kikuu cha kilimo wana programu inayokaribiana na hiyo ya Food science lakini sisi ya kwetu ni lishe moja kwa moja,” amesema

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Donald Mpanduji amesema mabadiliko ya mitindo ya maisha yanafanya watu kupata magonjwa mbalimbali ambayo yanazototesha utendaji.

“Kwa sababu yanahusu sana jamii tutakuwa tukitoa elimu kwa watu ili waweze kuzingatia lishe bora katika kuishi lakini pia walioathirika tayari tutawafundisha namna ya kujitibu kwa kutumia lishe,” amesema Profesa Mpanduji.

 

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz