Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Udart yataja sifa wanaotaka ajira za udereva wa mabasi yake

77509 Pic+udat

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Kampuni ya mabasi yaendayo haraka (Udart) imetangaza nafasi za kazi za madereva wa mabasi yake huku ikitaja sifa nane wanazopaswa kuwa nazo.

Kwa mujibu wa tangazo la kampuni hiyo, lililotolewa jana Septemba 26, 2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa Udart, mwombaji anapaswa awe na umri kati ya miaka 30 hadi 45.

Dereva anayehitaji nafasi hiyo anapaswa awe na leseni halali ya daraja C, mwenye uzoefu usiopungua miaka miwili.

“Awe na elimu ya darasa la saba na kuendelea, anayeweza kuandika taarifa za kazi yake kwa ufasaha. Awe na afya njema, akili timamu, ari ya kufanya kazi kwa tija, mwadilifu, mbunifu na anayeweza kujisimamia mwenyewe katika kutimiza majukumu atakayopewa,” imeelezwa.

Linaeleza kuwa dereva mwenye elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea ni sifa ya ziada lakini awe hajawahi kufanya kazi Udart.

“Barua za maombi ziambatane na CV, barua za wadhamini wawili kutoka Serikali ya Mtaa, kopi ya leseni, TIN na cheti cha mafunzo ya udereva. Kama anakidhi vigezo tajwa anapaswa kutuma maombi kabla ya Oktoba 15, 2019 na barua zote za maombi zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji,” linaeleza tangazo hilo.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz