Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Udanganyifu wa mitihani wawaponza 10 Chemba

20648 PIC+CHEMBA TanzaniaWeb

Thu, 4 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, jijini Dodoma, Dk Semistatus Mashimba amewavua madaraka walimu wakuu watano na waratibu elimu kata watano kwa tuhuma za kujihusisha katika udanganyifu wa mitihani ya darasa la saba.

Akizungumza ofisini kwake leo Oktoba 3, 2018,  Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amesema kuwa kwa mamlaka ya mkurugenzi huyo amewavua madaraka wakuu wa idara watano na wakuu wa shule watano kutokana na tukio hilo.

Akielezea tukio hilo, Odunga amesema wanafunzi wakiwa wanaendelea na mitihani walipata habari kutoka Shule ya Msingi ya Farkwa kuna udanganyifu wa mitihani na hivyo kamati ya mitihani kwenda huko.

Mkuu huyo wa wilaya amesema wilaya hiyo ina jumla ya shule 103 na wanafunzi 5362 waliochukuliwa hatua ndio waliobainika.

Amesema walipokwenda walibaini kuwapo kwa tukio hilo na hivyo wakachukua simu zao na wakaitaarifu kamati ya mitihani ya mkoa ambao walianza ufuatiliaji wa karibu wa tukio hilo.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na baada ya kukamilika wahusika watachukuliwa hatua za kisheria ukiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani

Amewataka wazazi kuhakikisha kuwa watoto wanakuwa wilayani Chemba kwa ajili ya kufanya mitihani Oktoba 8, 2018 na watapita kuwatangazia wazazi juu ya uamuzi huo.

Chanzo: mwananchi.co.tz