Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Udanganyifu wa mitihani wang’oa vigogo

Thu, 4 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Ofisa Elimu Halmashauri ya wilya ya Chemba na Ofisa Elimu Halmashauri ya wilaya ya Kondoa mji wamevuliwa vyeo vyao.

Hatua hiyo imekuja baada ya shule za msingi zote katika wilaya ya Chemba na shule moja iliyopo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma kufutiwa mitihani ya darasa la saba kutokana na udanganyifu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge, leo Oktoba 3, 2018 ameawaambia waandishi wa habari kuwa wamewavua pia madaraka makatibu wa elimu ngazi ya kata watano.

"Kutokana na udanganyifu huo pia walimu wakuu wa shule tano waliobainika wazi wazi katika hatua za awali za uchunguzi kujihusi na njama hizi wamesimamishwa,"

"Waalimu wanne waliokuwa wasimamizi wa mitihani katika shule binafsi ya Kondoa Integrity nao wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi,",amesema Dk, Mahenge.

Kutoka na tuhuma hizo Dk, Mahenge ameagiza Mamlaka za nidhamu kuwafungulia mashtaka wale wote waliohusika na tukio hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz