Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubungo yaibuka kinara Huduma Bora za Afya Dar es Salaam

Mkuu Wa Wwilaya Ya Ubungo, Henry James Ubungo yaibuka kinara Huduma Bora za Afya Dar es Salaam

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kupitia Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati wameibuka washindi na kupatiwa tuzo ya heshima katika utoaji wa huduma Bora za Afya Kati ya Halmashauri tano za mkoa huo katika kipindi cha mwaka 2021/2022.

Ubungo imeshika nafasi ya kwanza kwa kupata alama 237 ikifuatiwa na Halmashauri ya Temeke ikiwa na alama 236 na Halmashauri ya Kigamboni imeshika nafasi ya tatu kwa kupata alama 235.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao Cha Mwaka Cha Siku mbili kilicholenga kupata tathimini ya utendaji kazi wa sekta ya Afya Mkoa wa Dar es salaam, Katibu Tawala wa Mkoa huo Hassan Abbas Rugwa amepongeza sekta ya Afya kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika utoaji wa huduma Bora za Afya.

Aidha, Rugwa ametoa zawadi kwa Hospital ya rufaa ya Amana kwa kushika nafasi ya kwanza Kati ya hospital tatu za rufaa kwa kupata alama 118 ambapo Hospital ya rufaa Temeke imeshika nafasi ya pili kwa kupata alama 107 hospital ya rufaa Mwananyamala imeshika nafasi ya tatu na kwa kupata alama 102.

Pamoja na hayo Rugwa ametoa zawadi ya vyeti kwa Halmashauri zilizofanya vizuri katika kipengele Cha uandaaji wa mipango ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeshika nafasi ya kwanza kitaifa ya kwanza kimkoa, ikifuatiwa na Halmashauri ya Kinondoni nafasi ya pili kitaifa na ya pili kimkoa na Kigamboni nafasi ya tano kitaifa na tatu kimkoa.

Hata hivyo, Rugwa ametoa zawadi ya cheti kwa Amana Kituo cha kuwahudumia wagonjwa wa virusi vya UKIMWI pamoja na kwamba walifungiwa mwaka jana kutokana na UVIKO19 lakini bado wamefanya vizuri kuliko wengine huku akitoa vyeti kwa Ithibati ya kimataifa ya maabara kwa Hospitali ya Sinza Palestina, Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu, Hospitali ya Rufaa Temeke, Mwananyamala RRH, Amana RRH pamoja na Hospitali ya Mnazi Mmoja ambao Wameshinda kwa Mwaka huu.

Wakati huohuo, Rugwa ametoa zawadi kwa Manispaa zilizofanya vizuri kwenye kipengele Cha Usafi wa Mazingira ambapo Hospitali ya Rufaa Temeke imeshika nafasi ya kwanza kimkoa na nafasi ya pili kitaifa ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni iliyoshika nafasi ya pili kimkoa na nafasi ya tatu kitaifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live