Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UWT yataka wanafunzi wa kike kutochanganya mapenzi na masomo

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Queen Mlozi, amesema ana imani uamuzi wa Serikali kuwazuia wanafunzi wenye ujauzito kuendelea na masomo katika shule za Serikali unalenga kuandaa kizazi chenye kujitambua, kujiheshimu na kutekeleza majukumu kulingana na wakati.

Queen amesema hayo leo Jumatano Februari 27,2019 alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Ltd (MCL) Tabata jijjini Dar es Salaam akiwa katika ziara maalumu.

Amesema wanafunzi wasichana wanapaswa kutapambua wakati walionao na kile wanachopaswa kufanya ili waweze kuwa na mafanikio katika taaluma na hata kimaisha ya familia.

“Kila jambo lina wakati wake. Kwa utaratibu wetu hapa nchini kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita hapo mwanafunzi anapaswa kujikita katika masomo na kuacha mambo mengine.”

“Vijana wakiume wanapaswa kuwa msaada katika hilo kwa kuwaacha wasichana wasome ili wafikie malengo yao. Wale watakaokiuka na kuwapa ujauzito sheria ichukue mkondo wake,” amesema.

Akizungumzia hali ya kisiasa hususani kwa vyama vya upinzani amesema ni nzuri kwa kuwa kila mmoja anapata fursa ya kufanya shughuli zake bila ya kuingiliwa ikiwa atazingatia sheria na taratibu.

“Wanaolalamika huenda ni wale wanaokiuka sheria na taratibu. Mbona mimi kiongozi wa chama kitaifa nazunguka nchi nzima na kufanya mikutano ya ndani lakini sijawahi kuingiliwa wala kuzuiwa,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz