Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UWT kumuenzi Bibi titi Rufiji

UWT  RUFIJI (600 X 321) UWT kumuenzi Bibi titi Rufiji

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) itakayofanyika katika eneo la Ikwiriri Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani Oktoba 23 Mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari hii leo, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudentia Kabaka amesema maadhimisho hayo yamepangwa kufanyika Wilayani Rufiji kwa lengo la kuenzi mchango wa Mwenyekiti wa kwanza wa UWT na mpigania Uhuru wa Tanganyika, Bibi Titi Mohamed.

Kabaka amesema ahadi ya kufanyika kwa maadhimisho hayo wilayani Rufiji waliitoa katika kampeni za Urais mwaka 2020.

" Kilele Cha Wiki ya UWT kimelenga kumuenzi Mwanamke Shujaa na mpigania Uhuru wetu, Bibi Titi Mohamed ambaye Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere alimuona anafaa kumsaidia Kwenye mapambano ya Uhuru na kumchukua kazi ambayo aliifanya kwa weledi na nguvu kubwa.

Lakini pia tumechagua mgeni rasmi awe Rais Samia kwa sababu hii ni mara ya kwanza kupata Rais na Mwenyekiti wa CCM Mwanamke tena akiwa shupavu na Shujaa kama Bibi Titi,"

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakary Kunenge amemshukuru Mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudentia Kabaka kwa kuridhia maadhimisho hayo kufanyika Mkoani Pwani na hasa katika Wilaya hiyo ya Rufiji kwa lengo la kumuenzi mpigania huru huyu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live