Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNYAMA: Awachoma wanae kisa kula kwa majirani (+Video)

Unyama Njombe Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Adelina Ngolo (36) Mkazi wa Kijiji cha Nyombo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kuwachoma moto sehemu mbalimbali za mwili Watoto wake wawili na kuwasababishia madhara makubwa kwa madai ya kuwa wamekuwa wakimdhalilisha kutokana na kuomba chakula kwa Majirani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema Watoto hao waliojeruhiwa ni Eliud Chatanda (7) na Elina Chatanda (4).

“Sababu ya kuwachoma moto Watoto hawa yeye hakuwa makini na kuwaangalia hawa Watoto na kusababisha wawe wanatembea kwa Majirani na kuomba chochote kile ili siku iende na Majirani wakamwambia malezi ya Watoto sio hivyo kumbe Mama huyu anaweka moyoni na alipofika nyumbani kwake nyakati za usiku aliwaamsha na kuwachoma kwenye jiko la mafiga matatu”

Kamanda Issah ametoa wito kwa Wananchi kulea Watoto katika misingi inayokubalika na kuacha ukatili dhidi ya Watoto na sasa sheria ituchukuliwa dhidi ya Mwanamke huyo kutokana na ukatili alioufanya.

View this post on Instagram

A post shared by Geah (@geahhabib)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live