Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UCSAF yawakumbuka yatima

7050f9256792306f1c75b91b84ddead5 UCSAF yawakumbuka yatima

Sun, 7 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), umetoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Shillingi milioni 4.5 kwa watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu wanaolelewa katika Nyumba ya Matumaini Miyuji Jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa (UCSAF), Justina Mashiba, alisema wameamua kutoa mchango huo kama taasisi kwaajili ya kuchangia huduma mbalimbali zinazotelewa katika kituo.

Alisema kupitia Mfuko huo wameona ni vyema kwa kipindi hiki cha sikukuu ya wanawake duniani kuweza kujitoa kwa kuwaletea mahitaji hayo ikiwemo chakula, mafuta, na mahitaji mengine ya kike na kiume.

“Sisi kama wazazi tunawajibu wa kuwahudumia watoto wetu pasipo kujali ni wakuwazaa wenyewe ama lah, hivyo tuliamua kukusanyika kama Mfuko wa Mawasiliano kwa pamoja hususani wiki hii ni siku wa wanawake duniani hivyo tuje kituoni hapa kuwapatia chochote watoto hawa.”

Kwa upande wake Mlezi wa Kituo hicho cha Nyumba ya Matumaini, Sista Olea Kyala, alisema anaishukuru sana taasisi hiyo kwa moyo walio uonesha kwa kujitoa katika kuwasaidia watoto hawa na aliwaomba waendelee na moyo huo huo kuwasaidia watitaji wengine kwenye vituo mbalimbali hapa Nchini.

Chanzo: www.habarileo.co.tz