Fri, 30 Sep 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Gari lenye namba za usajili T 863 AGU lililokuwa linatokea Morogoro kuelekea Mikumi limemgonga Twiga hadi kufa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kisha gari hilo kupinduka.
Ajali hiyo imetokea jana, Septemba 29, 2022 katika Hifadhi ya Taifa Mikumi karibu na geti kuu la kuingilia kwenye Hifadhi hiyo Barabara Kuu ya Morogoro - Iringa.
Dereva wa Fuso ambaye jina lake bado halijafahamika amejeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya St. Kizito Mikumi kwa ajili ya matibabu.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live